Saturday 19 September 2015

Mwana AMANI Prince Muumini Mwinjuma 'Kocha wa Dunia' aendeleza libeneka akiwa Msumbiji

  Vijana wa Mwana AMANI mwanzilishi Prince Mwinjuma Muumini 'Kocha wa Dunia' wakiwa kazini na vijana wake huko katika mji wa madini wa Mount Pwesh Msumbiji
  Mwana AMANI mwanzilishi Prince Mwinjuma Muumini 'Kocha wa Dunia' akiwa kazini na vijana wake huko katika mji wa madini wa Mount Pwesh Msumbiji
 Mwana AMANI mwanzilishi Prince Mwinjuma Muumini 'Kocha wa Dunia' akiwa kazini na vijana wake huko katika mji wa madini wa Mount Pwesh Msumbiji
 Kocha wa dunia na vijana wake wakiwa kazini Msumbiji
 Ma Dancer wa Prince Muumini wakiwa kazini Mount Pwesh
Sebene la nguvu likitawala Mount Pwesh

RADIO EFM 93.7 YAAFIKI USHIRIKIANO NA AMANI KWANZA GROUP

Mratibu wa AMANI KWANZA GROUP Ankal Michuzi akiwa na Dennis Ssebo wa EFM 93.7 baada ya kikao chao ambapo kituo hicho cha redio inayokuja juu sana nchini kukubali kushirikiana na AMANI KWANZA GROUP katika kuendeleza wimbi la ushirikiano kati ya wanamuziki wakongwe na vijana. Tayari EFM imetoa mwaliko kwa wana AMANI KWANZA kushiriki katika nusu fainali za MUZIKI MNENE wa kituo hicho Oktoba 10, 2015 huko Kigamboni, ambapo wakongwe watapanda jukwaani kwa mara ya kwanza.

Inspekta Haroun afurahia mikakati ya AMANI KWANZA GROUP

Msanii Inspekta Haroun akisalimiana na wajumbe wa AMANI KWANZA GROUP alipowakuta katika kikao chao cha kwanza Leaders Club jijini Dar es salaam Ijumaa Septemba 18, 2015, ambapo alifurahi kusikia mipango ya kundi hilo la wanamuziki wakongwe ya kuunganisha nguvu na wanamuziki vijana ili kuendeleza tasnia hiyo Tanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda abariki ujio wa AMANI KWANZA GROUP

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda akiwasalimia wajumbe wa mkutano wa kwanza wa AMANI KWANZA GROUP alipowakuta wakiwa mkutanoni Leaders Club Ijumaa Septemba 18, 2015. Mhe. Makonda, ambaye ni kiomgozi wa mfano mwenye kupenda maendeleo, aliubariki mpango mzima wa AMANI KWANZA GROUP wa kuuganisha nguvu kati ya wanamuziki wakongwe na vijana kwa kuahidi kuusaidia umoja huo wa waina yake kwa hali na mali.

UONGOZI WA AMANI KWANZA WAPATIKANA

Mratibu wa AMANI KWANZA Ankal Michuzi akiwa na Mwenyekiti Kanku Kelly, Katibu Faliala Mbutu, Katibu Msaidizi Mjusi Shemboza na Makamu wa Mwenyekiti Mafumu Bilali Bombenga kabla ya kuanza kikao cha kwanza ch AMANI GROUP  katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.

Baada ya kukubaliana kufanya kikao rasmi cha kuunda AMANI KWANZA Group, wajumbe walikutana kwa chakula cha mchana na mkutano katika mgahawa wa Leaders Club jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa ya tarehe 18 Septemba 2015.

Katika kikao hicho kukafanyika uteuzi wa viongozi wa kuendeleza mpango mzima wa AMANI KWANZA GROUP kama ifuatavyo.

1. Mwenyekiti - Kanku Kelly
2.Makamu Mwenyekiti - Mafumu Bilali Bombenga
3. Katibu - Faliala Mbutu
4. Katibu Msaidizi - Mjusi Shemboza
5. Mhazini - Luiza Mbutu
6. Afisa Mipango - Komandoo Hamza Kalala
7. Mratibu - Muhidin Issa Michuzi

AMANI KWANZA GROUP YAZALIWA

Mratibu wa AMANI KWANZA Muhidin Issa Michuzi akiwa na wanamuziki nyota wa Tanzania - Cassim Mganga wa Bongo Fleva na Hassan Rehani Bitchuka 'Stereo' katika viwanja vya Leaders  Club jijini Dar es salaam Ijuma Septemba 18, 2015. Hii ikiwa ni mwanzo mzuri na mwendelezo wa dhamira ya kundi la AMANI KWANZA la kuunganisha vipaji vya kale na vya sasa.
Nyota wa Bongo Fleva Cassim Mganga akiwa na gwiji la uimbaji Tanzania Hassan Rehani Bitchuka 'Stereo' 

Awali ilianza kama kundi la wanamuziki wakongwe nchini Tanzania waliojikusanya ili kutunga wimbo wa kuhamasisha amani wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, na baada ya uchaguzi huo. 

Walipofanikisha hilo, wanamuziki hao wakakaa na kutafakari. Je, baada ya wimbo huu nini kifuatie?
Ndipo likaja wazo la kuudumisha umoja huo kwa kuanzisha kunzi la wanamuziki, wakongwe na vijana, ili kuweka sawa mustakabali wa muziki wa Tanzania.

Hivyo azma mama ya AMANI KWANZA GROUP ni kuwaunganisha wanamuziki wakongwe na vijana ili kuziba ombwe kubwa lililopo, ambapo kwayo kumesababisha mfarakano usio wa lazima, kwani duniani kote wanamuziki wakongwe na vijana sasa wanaungana na kufanya kazi pamoja. Sembuse Tanzania?

Hayawai hayawi sasa yamekuwa. Wanamuziki wakongwe sasa wameamka na kuamua kurithisha vipaji vyao kwa wanamuziki vijana, maarufu kama BONGO FLEVA. Makubaliano ni kwamba kuanzia sasa wanamuziki wakongwe watashikamana na wanamuziki vijana ili kukuza tasnia hii.

Hakuna safari isiyo na changamoto zake. Ile sintofahamu iliyopo baina ya wanamuziki wakongwe na vijana lazima itajitokeza sana. Upande mmoja ukisema wazee ni wazee na wakati wao umepita, na vijana wakisema wakongwe hawana jipya, hiyo ikiwa ni KOSA moja kubwa sana ambalo wanamuzki wa Tanzania wanafanya.

Piga ua, lakini kila upande hapo unategemea mwenzake. Muungano huu wa wakongwe na vijana unaashiria mambo mazuri kwa tasnia ya muziki Tanzania. Kilichokosekana awali sasa kimepatikana.
Wakongwe na vijana watakuwa kitu kimoja kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.

IDUMU AMANI KWANZA!